Gavana wa Mombasa Hassan Joho akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Photo/ the-star.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho amesisitiza kuwa ataendeleza juhudi za kujitenga kwa eneo la Pwani.Akizungumza siku ya Jumapili kwenye kongamano la viongozi wa muungano wa NASA katika hoteli moja Kaunti ya Kilifi, Joho alisema kuwa mchakato wa eneo hilo kujitenga unazidi kupamba moto.Joho alisema kuwa sharti wakaazi wa Pwani wajitenge ili waweze kunufaika na raslimali ya eneo hilo vyema.“Lazima Pwani tujitenge ili tuweze kuwahudumia wapwani vyema," alisema Joho.Gavana huyo alisema kuwa Wapwani wengi hawana ajira na wametengwa kimaendeleo kwa muda mrefu.“Wapwani wengi hawana ajira tangu jadi kwa kuwa wametengwa kimaendeleo kwa muda mrefu," alisema Joho.Kwa upande wake, Gavana wa Kilifi Amason Kingi alisema kuwa kujitenga kwa eneo hilo kutaendeleza vyema raslimali na kuwafaidi wengi.Kingi aliilaumu serikali kuu kwa kutenga eneo la Pwani na kukosa kukabiliana na umaskini miongoni mwa wakaazi.Haya yanajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa onyo kwa viongozi wa NASA kwa kusema kuwa yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria atakabila na mkono wa sheria.Rais Uhuru alisema kuwa eneo la Pwani litaendelea kuwa Kenya na haliwezi kujitenga kamwe.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6