Mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung'aro amepuzilia mbali maadai kuwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho ndiye kiongozi mkuu wa kanda ya Pwani.
Mung'aro ambaye alikuwa katika ziara ya kukutana na wakaazi wa eneo bunge lake siku ya Alhamisi alisema kuwa Joho hawezi unganisha kaunti zote za Pwani ikiwa ameshindwa kuunganisha Kaunti ya Mombasa.
“Sisi hatuwezi muunga mkono mtu ambaye hana nia nzuri kwa watu wa Pwani ila kujinufaisha yeye binafsi,” alisema mbunge huyo.
Aidha, Mung'aro aliahidi kuendelea kufanya kazi na serikali ya Jubilee kwa kuleta maendeleo katika eneo bunge lake.
Mbunge huyo aliongeza kuwa hivi karibuni yeye pamoja na wabunge wengine ambao wameasi mrengo wa Cord watatangaza ni chama gani watatumia katika uchaguzi mkuu ujao.