Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho amesema kuwa amewasilisha ombi kwa wafadhili kadhaa kutoka humu nchini na hata wa kimataifa ili kuisadia kaunti hiyo katika miradi ya maendeleo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wawakilishi wa maendeleo katika wadi afisini mwake siku ya Jumanne, Gavana Joho amesema kuwa miradi ambayo kamati yake ya mawaziri imependekeza kufanyika katika kaunti hiyo itagharimu pesa nyingi na hivyo ni lazima wawashirikishe wafadhili.

Baadhi ya miradi aliyotaja gavana huyo ni pamoja na ujenzi wa vyumba, kununua vifaa vya hospitali na ujenzi wa barabara katika wadi mbali mbali.

“Kuna wasamaria wema ambao wangetaka kuona kaunti yetu ikipata maendeleoa na sisis tunawakaribisha ili tuweze kufanya kazi pamoja na kutumikia wakaazi wa kaunti ya Mombasa,” alisema Joho.