Huenda gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho akajipata katika hali ya njia panda baada ya maafisa wakuu serikalini mwake kutangaza kuwania nyadfa mbali mbali za uongozi pindi uchaguzi mkuu utakapowadia.
Kulingana na mchanganuzi wa maswala ya kisiasa katika eneo la Pwani wakili Johnson Muchiri, hatua hiyo ni pigo kubwa sana kwa gavana huyo aliyetangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Kwenye mahojiano ya kipekee na mwanahabari huyo afisni mwake mjini Mombasa siku ya Jumatatu, wakili Muchiri amesema kuwa iwapo maafisa hao watashikilia azma yao ya kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi basi huenda umaarufu wa gavana huyo unapungua kwani maafisa hao ni wandani sana wa gavana huyo.
“Madai kuwa baadhi ya maafisa wakuu wa serikali ya gavana Joho kutangaza kuwania nyadhfa za uongozi wakati wa uchaguzi mkuu ujao, hatua hiyo ni pigo kubwa sana kwa gavana huyo na huenda umaarufu wake wa kisiasa ukapungua kufuatia maafisa hao kuwa wandani wa karibu wa gavana Joho,” alisema Wakili Muchiri.
Akigusia swala la kisaisa za Pwani, mchanganuzi huyo wa kisiasa amesema kuwa siasa za pwani zinahitaja kiongozi wenye uwezo wa kuwaunganisha wapwani wote lakini sio baadhi ya makabila na akasema kuwa gavana Joho ana kazi kubwa kwani bado hajakubaliwa na jamii yote ya Pwani hivyo basi kuwa rais wa taifa hili sio rahisi.
“Joho ana kazi kubwa ya kuwaunganisha Wapwani mwanzo kabla ya kutangaza kuwania urais kwa bado hajakubaliwa katika jamii yote ya pwani ni baadhi tu ya makabila fulani na yeye kuw rais lazima akubalike Kenya nzima sio kaunti ya Mombasa pekee,” aliongeza Muchiri.
Kuali ya Muchiri inajiri baada ya waziri wa Elimu kaunti ya Mombasa Tendai Lewa Mtana na Katibu wa Baraza la Mawaziri Khamis Mwaguya kutangaza kuwania nyadhfa za uongozi huku mwaguya akijuhulu katika serikali ya gavana huyo.