Gavana wa Mombasa Hassan Joho akiwahutubia wanahabari hapo awali. Ameagiza wanachama wote wa ODM eneo la Kwale kuunganana ili kuhakikisha viongozi waasi hawapati kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti. Picha/mediamaxnetwork.co.ke

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Mombasa Hassan Joho amewataja wanasiasa walioasi mrengo wa Cord na kujiunga na Jubilee kama viongozi wabinafsi.

Joho amewashtumu viongozi kutoka Kaunti ya Kwale waliohamia upande wa serikali, na kusema kuwa hatua hiyo inaonyesha udhaifu wao hasa wakati huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia.“Viongozi hao wamefata maslahi yao binafsi wala sio ya wananchi. Walidanganywa na wataanguka kwenye uchaguzi ujao,” alisema Joho.Gavana huyo ameagiza wanachama wote wa ODM eneo la Kwale kuunganana ili kuhakikisha viongozi waasi hawapati kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti.Joho alisema kuwa lazima Kwale ibaki kuwa ngome ya ODM.Aidha, amewataka viongozi wa ODM kuwa na msimamo thabiti na kuhakikisha Jubilee inabanduliwa mamlakani.Joho amewahimiza viongozi wa ODM kutosita kumweleza Rais Uhuru Kenyatta kuhusu jinsi serikali yake ilivyofeli katika uongozi.Baadhi ya viongozi kutoka Kwale waliojiunga na Jubilee ni Gavana Salim Mvurya, Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani na mwakilishi wa wanawake Zainab Chidzuga.