Baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang, viongozi mbalimbali wamejitokeza kupongeza uamuzi wa mahakama hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar amesema kuwa mahakama hiyo ya ICC ilichukua uamuzi wa busara ili kusitisha joto la kisiasa na uvumi uliyokuwa ikidiwa kuchochea wananchi kuzua vurugu na kuharibu uchuguzi mkuu ujao.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Omar amesema kuwa sasa ni wakati wa Ruto kuondoa hofu na kufanya kazi kwa karibu mno na viongozi wa taifa hili ili kuwafanyia wakenya maendeleo.

Amesema kuwa joto la kisiasa na kikabila lililokuwa likikisiwa kuzuka pia nalo limezikwa katika kabura la sahau na kilichosalia sasa ni wakenya kuungana na kudumisha amani sambamba na kuwashinikiza viongozi kukamilisha miradi waliyokuwa wameahidi kwa wakemnya.

"Kushinda kwa Ruto na Sang tunaimani kuwa amani na utangamano utazidishwa zaidi, na joto la kisiasa pia litasitishwa kwa sababu tayari tumekuwa tunaanza kuona siasa za ukabila na chuki zikianza lakini sana tunamatumani kuwa tutafanya kazi kwa pamoja na serikali," alisema Omar.

Kauli ya Kiongozi huyo imejira baada ya kesi ya maauji ya watu zaidi ya elfu moja wakati wa ghasia za baada ya uchuguzi mkuu wa mwaka wa 2007/2008 iliyokuwa ikimkabilia naibu Rais William Ruto na Mwanahabari Joshua Sang kutupiliwa mbali na majaji wa mahakama ya ICC.

Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar Sarai, akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamisi. Amesema kuwa sasa ni wakati wa Ruto kuondoa hofu na kufanya kazi kwa karibu mno na viongozi wa taifa.