Mwanasiasa Peterson Mitau amesema kuwa chama cha Jubilee hakiwezi shinda kiti chochote katika Kaunti ya Mombasa na eneo la Pwani kwa jumla.
Mitau, ambaye ni mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo la Changamwe, alisema kuwa kampeni zinazoendelezwa na chama cha Jubilee katika ukanda wa Pwani zinadhihirisha kushindwa kwa chama hicho ifikapo uchaguzi mkuu.Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Mitau alisema kuwa mrengo wa NASA uko imara katika ukanda wa Pwani.Mwanasiasa huyo alisema ana imani kuwa mrengo huo wa upinzani utapata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.Wakati huo huo, Mitau amewataka wakaazi wa ukanda wa Pwani kujiandikisha kama wapiga kura kwa wingi, kwa kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuwateua viongozi watakaoleta maendeleo.
Maelezo ya picha: Mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Changamwe Peterson Mitau katika hafla ya awali.
Picha/ the-star.co.ke