Viongozi wa Jubilee katika ukanda wa Pwani wamesema kuwa wanazidi kujipanga vilivyo kunyakua viti mbalimbali katika uchaguzi wa mwezi Agosti.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa chama cha Jubilee Kaunti ya Mombasa Ali Mwatsahu amesema chama hicho kitaonyesha umaarufu wake katika uchaguzi ujao kutokana na kuongezeka kwa idadi ya viongozi wanaohamia chama hicho kutoka vyama vingine.

Mwatsahu amewataka wakaazi wa Mombasa na ukanda mzima wa Pwani kujitenga na kasumba kuwa eneo hilo ni ngome ya mrengo wa Cord.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa fikra kama hizo zimepitwa na wakati kwani Jubilee itanyakua viti mbali mbali katika uchaguzi ujao.

Aidha, aliwataka wakaazi kujitenga na siasa za vyama, na kuongeza kuwa viongozi wanapaswa kuteuliwa kulingana na maendeleo waliyoletea wananchi.

“Ningependa kuwahimiza wakaazi kuwa wangalifu tunapoelekea kipindi cha uchaguzi. Tuwachague viongozi wanaostahili bila kuegemea chama chochote kwani siasa za vyama ndizo zilizopelekea ukanda wa Pwani kubaki nyuma kimaendeleo,” alisema Mwatsahu.