Naibu Rais William Ruto amesema serikali ya Jubilee itaimarisha zaidi sekta ya afya ata ingawa iko chini ya usimamizi wa serikali za kaunti ili wananchi kupata huduma bora za matibabu kikamilifu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Kebirigo, kaunti ya Nyamira, Ruto alisema lengo la serikali kuu ni kufanikisha maendeleo, huku akisema sekta ya afya itaimarishwa zaidi

Wakati huo huo, Ruto alisema hospitali zote zitakuwa na huduma bora za matibabu huku akisema ukarabati wa barabara utawezeshwa zaidi ili kurahisisha sekta ya uchukuzi nchini.

“Mnaona leo hospitali ya Nyamira imekabidhiwa na mashine mbalimbali za matibabu, lile tunahitaji ni kuhakikisha huduma za afya ziko shwari kote nchini,” alisema Ruto

“Ukarabati wa barabara nao hautasaulika tunahitaji kila mkenya kufurahia uongozi wa serikali iliyoko mamlakani,” aliongeza Ruto.

Wakati huo huo, Ruto aliomba wakazi wa jamii ya Kisii kushirikiana na kuungana na serikali ya Jubilee ili kufaidika zaidi kimaendeleo huku akisema lengo la serikali ya Jubilee ni kuleta maendeleo zaidi kwa wananchi wote.