Mweyekiti wa Jomo Kenyatta Foundation amesema kuwa serikali ya Jubilee imejitolea kufanya maendeleo katika sehemu za Kisii na katika sehemu zingine nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na wanahabari mjini Kisii, Walter Nyambati alisema kuwa serikali ya Jubilee inalenga kutimiza manifesto yao kabla ya uchaguzi mkuu ujao, kwa kuhakikisha maendeleo yamefanywa katika kila sehemu humu nchini.

“Serikali yetu ikiongozwa na Rais Kenyatta itahakikisha kuwa inatimiza ahadi zake. Tayari Rais Kenyatta amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Kisii na katika sehemu zingine nchini. Jubilee itaendelea kuleta maendeleo kwa waakazi,” alisema Nyambati.

Aidha, Nyambati aliwahimiza wakaazi wa Kisii kuombea nchi ya Kenya iwe na amani ili taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo na kufaidi Wakenya wote kwa ujumla.

Nyambati pia aliomba jamii ya Kisii kuendelea kuunga mkono serikali ya Jubilee ili kufaidika zaidi.

“Hakuna haja ya kutofanya kazi na serikali. Sharti sisi sote tuwe kitu kimoja ili kujenga taifa letu,” alisema Nyambati.