Raisi Uhuru Kenyatta. [Photo/kbc.co.ke]Serikali ya Jubilee imelaumiwa kwa kushindwa kutatua tatizo la ardhi linalowakumba wakazi wengi eneo la Kwale, Mombasa na Pwani kwa ujumla.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na wakazi wa Msambweni, mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori, amesema Jubilee imefumbia macho maswala muhimu ambayo inafaa kuwatekelezea wakazi wa Pwani kama vile ardhi,barabara na maji.

“Mashamba yetu yako na shida nyingi za umiliki,serikali ya jubilee imetusahahu kwa hilo kwa mda mrefu sana," alisema Dori.

Ameongeza kuwa idadi kubwa ya wa Pwani ni maskota na hawajui watapata umiliki kamili wa mashamba yao lini.

“Maelefu ya wapwani wanaishi kama maskota,hawana umiliki halali wa ardhi zao,tunasikitishwa n asana na hatua hii," alisema Dori.

Dori amesisitiza kuwa hadi kufikia sasa umiliki wa ardhi umebakia kuwa ndoto tu kwa wapwani licha ya serikali ya jubilee kujigamba kwamba itahakikisha imemaliza uskwota pwani.

Kando na hayo mbunge huyo ameshtumu Gavana wa Kwale Salim Mvurya kwa kukosa kuungana na viongozi wa NASA waliochaguliwa kwa minajil ya maendeleo badala yake kuungana na jubilee kuendelea kuwahadaa Wapawani.

Ni kauli iliyopigiwa upato na Spika wa bunge la  Kwale Sammy Ruwa aliyetaja kukithiri kwa ufisadi ndani ya serikali ya jubilee kutokana na  ubadhirifu  wa mabilioni ya fedha za umma.