Kinara mwenza wa Nasa Kalonzo Musyoka.[barakafm.org]Kinara mwenza wa muungano wa Nasa Kalonzo Musyoka ameilamu serikaili ya Jubilee kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya elimu bila malipo kama inavyostahili.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kalonzo amesema kuwa bado wazazi wanaopeleka watoto wao katika  shule za kitaifa wanakumbwa na mzigo mkubwa wa kulipa karo.

Akizungumza jijini Mombasa wakati wa uzinduzi wa bunge la wananchi siku ya Jumapili, Kalonzo alisema ingekuwa bora iwapo wanafunzi wa shule za kitaifa wasingelipa hata shilingi katika shule hizo.

Alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kutoka jamii maskini ambao walipaswa kujiunga na shule za kitaifa bado wanataabika licha ya Jubilee kusema kuwa imefanikisha elimu bila malipo.

“Watoto wengi waliofanya vyema na walistahili kujiunga na shule za kitaifa bado wamesalia kudubwa kwa sababu wazazi hawana uwezo wakulipa karo zinazohitajika,licha ya mpango wa elimu ya bure wa Jubilee," alisema Kalonzo.

Ameitaka Jubilee kuondoa karo zozote katika shule za kitaifa kote nchini ili wanafunzi kutoka jamii maskini waweze kujiunga na shule hizo za kitaifa.