Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mali ya thamani ya milioni imeteketea usiku wa kuamkia Alhamis katika eneo la Mtwapa baada ya jumba lijulikanalo kama Funyula kushika moto.

Kulingana na waliyoshuhudia kisa hicho wamesema kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa tatu usiku bila ya kufahamu chanzo halisi cha moto huo.

Wahudumu wa jumba hilo la kibiashara wamesema kuwa wazima moto kutoka serikali ya kaunti ya Kilifi na Mombasa pamoja na kampuni ya Radar kutoka eneo la Shanzu walipata wakati mgumu kuuzima moto huo ambao ulichukua masaa matatu kuzimwa.

Akithibitisha mkasa huo mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Joshua Ole Leina aliyefika katika mkasa huo amesema kuwa jumba hilo linamilikiwa na Margeret Tabu Mzungu aliyepoteza jumla ya shilingi milioni 30 kufutia mkasa huo.

“Hii ni hasara kubwa sana kwa mmiliki wa jumba hili na serikali kwani idadi kubwa ya wakazi wanaofanya kazi hapa watakosa ajira na kwa hivyo lazima watu wawe waangalifu, tunachunguza mkasa huu na tutatoa ripoti kamili baada ya kubaini chnazo cha moto huu nini, alisema Ole Leina.

Ameongezea kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa licha ya kukosa kuokoa mali iliyokuwa ndani ya jumba hilo