Chama cha Kadu Asili tawi la Pwani kimekanusha madai ya kuhusishwa na kundi la kihalifu la Kadu Asili Networks.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kundi hilo ni miongoni mwa makundi yaliyowekwa katika gazeti rasmi la serikali kama makundi hatari.

Kinara wa chama hicho Gunga Mwinga, amemtaka Waziri wa usalama Joseph Nkaissery kueleza zaidi kuhusu kundi hilo ambalo jina lake linafana na jina la chama hicho cha kisiasa.

“Itabidi Waziri Nkaissery atuelezee kwa kina kuhusu mizizi ya kundi hili ambalo huenda likahujumu juhudi za chama cha Kadu Asili,” alisema Gunga.

Gunga aidha alisema hali hiyo huenda ikawa ni njama ya serikali ya kujaribu kuhujumu juhudi za chama hicho za kuendeleza siasa zake hapa nchini.

Orodha hiyo ilitolewa mnamo Desemba 30, mwaka jana, ambapo makundi hayo yalidaiwa kuwa hatari kwa usalama wa nchi.

Miongoni mwa makundi hayo ni 42 brothers, Akili za usiku, Gaza, Lipa kwanza, Islamic state miongoni mwa makundi mengine.