Waziri wa Ardhi Jacob Kaimenyi katika hafla ya awali. [Picha/ nation.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri wa Ardhi Jacob Kaimenyi amefanya ziara ya kushtukiza katika afisi za usajili wa ardhi hapa Mombasa.

Akizungumzwa wakati wa ziara hizo siku ya Jumanne, Kaimenyi alisema kuwa hakuridhishwa na namna wafanyakazi hao wanavyoendesha shughuli zao.

“Sikupendezwa na jinsi wafanyakazi wanavyohudumu kwani wengi wao wanachelewa kufika kazini,” alisema Kaimenyi.

Aidha, alisema kuwa jumla ya watu watatu kati ya 19 ndio wanaofika afisini kwa wakati ufao.

“Nimekuta afisi hii ikiwa haina wafanyakazi wa kutosha licha ya muda wa kufika kazini kupita,” alisema Kaimenyi.

Aidha, alidokeza kuwa afisi hiyo haina ushahidi wa kuwa inaandaa mikutano yake.

Wakati huo huo, Kaimenyi amewataka wakaazi ambao hawajamaliza kulipa ada ya Shamba la Waitiki kumaliza malipo hayo ili wakabidhiwe hati miliki zao.

Kaimenyi alisema kuwa takriban asilimia 65 ya hati miliki za ardhi ya Waitiki eneo bunge la Likoni zimeshatolewa kwa wale waliomaliza malipo yao.

“Tayari tumetoa takribani asilimia 65 ya hati miliki kwa wakazi waliomaliza kulipa ada ya ardhi hiyo,” alisema Kaimenyi.

Kaimenyi aidha amewataka wanasiasa kutotumia suala la ardhi kujitafutia kura.