Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mgandi Kalinga ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 ama pesa taslimu shilingi 100,000 kwa kosa la utumizi mbaya wa vyombo vya mawasiliano.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kalinga anadaiwa kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp, hasa katika kikundi cha Mombasa Community Forum, kumtusi seneta mteule kaunti ya Mombasa, Emma Mbura mnamo Machi 19, 2016.

Mwanaharakati huyo alitiwa mbaroni siku ya Ijumaa wiki iliyopita, baada ya kuenea sauti zilizorekodiwa zinazohusisha wawili hao kimapenzi.

Siku ya Jumatatu, Kalinga aliiambia mahakama kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na seneta Mbura kwa muda mrefu mpaka ukavunja uhusiano wake wa ndoa na mke wake wa kwanza.