Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akicheza na kinara wa Nasa Raila Odinga.[barakafm.org]

Share news tips with us here at Hivisasa

Kinara mwenza wa muungano wa Nasa Kalonzo Musyoka amewataka vinara wa chama cha  ODM kuzingatia usawa katika ugavi wa nafasi za uwakilishi katika kamati mbali mbali za bunge.

Akizungumza jijini Mombasa siku ya Jumapili wakati wa uzinduzi wa bunge la wananchi, amsema kuwa licha ya kuwa Odm inafaa kuzingatia kuwa chama cha Wiper, Ford Kenya, ANC viko ndani ya Nasa na vinahitaji uwakilishi sawa katika kamati za bunge.

Ameitaja ODM kutojipatia nafasi hizo pekee na kusahau uwepo wa vyama vyengine ambavyo vinaunda mrengo wa NASA.

"Mimi niko hapa leo na ningependa kuwauliza wenzetu wa ODM wasijinyakulie kila kitu ndio pia Wiper wapate kidogo. Sisi tuko nyumba moja ya NASA kwa hivyo wacha zote tufurahie kuwa na mzazi mmoja sio?," alisema Kalonzo.

Kauli yake inajiri baada ya Wiper na ANC kukashifu namna ODM ilivyojipatia uwakilishi kwa wingi katika kamati hizo za bunge.