Viongozi wa mrengo wa upinzani, Cord wameshikilia msimamo wao kuwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka lazima waondolewe toka afisini kwa kuwa wakenya wengi hawana imani nao.
Akiongea katika futari iliyoandaliwa na sheikh Twaha Jaabali katika maeneo ya Bamburi, mmoja wa vinara wa mrengo huo Kalonzo Musyoka amesema kuwa mbali na tume hiyo kufurushwa, ni lazima pia shuguli ya uandikishaji wa kura kufanywa upya.
Aidha, Musyoka amekashifu vikali mauaji ya kiholela ambayo yameshuhudiwa humu nchini na kuitaka serikali kuwajibika ili kulinda wananchi, huku akiwataka wananchi kutokubali kugawanywa kwa msingi ya kikabila au za kidini na kuwataka jamii ya waislamu kuiombea nchi katika wakati huu wa kuadhimisha siku ya Eid.
Aidha, Kinara huyo wa Cord pia amesema kuwa ana imani kuwa mrengo wa Cord itamteua ili kupeperusha bendera ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.