Kamati ya kuchunguza utumizi wa pesa za serikali katika bunge la kaunti ya Kisii imeanza kutengeneza ripoti kamili kuhusu utumizi wa pesa za serikali katika bajeti ya mwaka 2014 /2015,  baada ya kamati hiyo kumaliza kuchunguza kuhusiana na utumizi wa fedha.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya baadhi ya viongozi wa kaunti hiyo na wakazi wengine kutaka ripoti hiyo kutolewa rasmi kuonyesha yale walikuwa wakiyachungunza kutoka kwa mawaziri hao

Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Kisii, mwenyekiti wa kamati hiyo Ronald Onduso alisema ripoti hiyo imeanza kutayarishwa na kuahidi kutolewa hivi karibuni.

Onduso alisema ripoti hiyo imechukuwa muda kutolewa kufuatia ukosefu wa pesa ambazo zingewawezesha wanakamati hao kutembelea miradi iliyofanywa katika kila wadi, huku wakisema watajaribu kila wawezalo kuhakikisha ripoti hiyo imetolewa ili wananchi kujua jinsi pesa za serikali zilitumika .

“Tutatoa ripoti hiyo ingawa tumechukua mda ni kwa sababu ya pesa za kutembelea miradi kila wadi zilikosa, lakini naomba wakazi kuwa na imani kwani ripoti hiyo itatolewa karibuni,” alisema Onduso.

Mwakilishi mteule katika kaunti hiyo ya kisii Irene Areri alikuwa wa kwanza kutaka kuona ripoti hiyo ili kujua jinsi pesa zilizotengewa walemavu zilitumika na kwa njia ipi.