Kamati ya usalama ya wilaya ya Naivasha imeonya kuwa mizozo ya kila mara ya ardhi katika eneo hilo huenda ikasababisha ghasia wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hadi sasa, watu wanne wameuawa katika kipindi cha mwezi mmoja katika eneo la Kosovo kufatia ghasia zanazotokana na umiliki wa ardhi.

Aidha, kumeibuka mizozo mipya kwenye ardhi itakakopitia reli ya kisasa ya SGR hususani maeneo kati ya Mai Mahiu, Kedong na Olkaria.

Mkuu wa wilaya ya Naivasha Isaac Masinde alisema kuwa kuna mizozo kumi na miwili inayohusisha kampuni za kununua ardhi.

“Tusipoishi kwa amani na utangamano na tutatue swala hili la ardhi mara moja huenda tukakumbwa na mizozo siku zijazo na haswa kwenye uchaguzi, naomba tuwe wastaarabu na tufanye mambo kisheria.” Alisema Bw Masinde.

Akizungumza baada ya kufungua kambi ya polisi eneo la Kosovo Jumatatu, Masinde ameonya pia wafugaji kuwa waheshimu ardhi za kibinafsi wanapotafuta lishe kwa wanyama wao.