Aliyekuwa Waziri wa Leba Kazungu Kambi amewataka wanasiasa kuacha siasa za chuki na badala yake kushirikiana na kuhudumia wananchi waliowachagua.
Akizungumza siku ya Jumapili wakati wa mazishi ya kakake Katana Ngala katika eneo la Kaloleni, Kambi alisema kuwa viongozi wengi wameacha majukumu yao ya kuhudumia wananchi na kujiingiza katika malumbano yasiyokuwa na msingi wowote.
Kambi aliwataka viongozi kuondoa siasa za chuki na kuwahudumia wananchi vyema katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi ili kukabiliana na umaskini.
Haya yanajiri baada ya kushuhudiwa viongozi wengi wakirushiana maneno ya chuki pasi kuimarisha maendeleo kwa wananchi.