Polisi katika kaunti ya Garissa wamenufaika baada ya juhudi zao za kuhakikisha usalama kupata msaada zaidi wa magari kumi ya usalama.
Magari hayo yatatumika katika harakati za kuhakikisha usalama kwenye Kambi ya wakimbizi ya Daadab.
Akizungumza alipokuwa akizundua magari hayo, kiongozi wa maeneo ya Garissa, Mohamud Saleh alisema kuwa magari hayo yatasaidia sana katika vita dhidi ya ugaidi. Alisema kuwa serikali imepata matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi na ya usalama kwa sababu ya wakimbizi wao kutoka Somalia.
“Serikali ya Kenya ikishirikiana na hhirika la umoja wa mataifa inayoshughulika na wakimbizi, (UNHCR) imetoa msaada ya magari haya ambayo yatasaidia katika kuleta usalama ya wenyeji na wakimbizi,’’ alisema Saleh.
Serikali imekuwa ikilalamikia kuwepo kwa kambi hiyo ya Daadab kwa sababu magaidi wameitumia kama sehemu ya maficho na uwanja wa kupangia njama zao za kigaidi kisha kuyatekeleza katika sehemu tofauti nchini. Hata hivyo, Saleh alipongeza juhudi za wenyeji na serikali, akisema kuwa ni kupitia ushirikiano yao ndio usalama umeimarika.
“Wakimbizi na wenyeji wamekuwa wa msaada sana kwa kutoa habari za dharura na kwa wakati kuwahusu washukiwa wa ugaidi, ambao wamekamatwa na afisa wa usalama,’’ aliongezea Saleh.
Magari yaliyozinduliwa yatatumiwa na polisi pamoja na polisi wa utawala.
Shughuli za kuzindua magari hayo yalishuhudiwa na mwakilishi wa UNHCR, Rauf Mazou na naibu wa gavana wa Garissa, Abdullahi Husein pamoja na afisa wengine wa kaunti ya Garissa.