Kamishna wa Kaunti ya Kisii Chege Mwangi amewahakikishia wakaazi wa Lokesheni ya Gesure wilayani Sameta kuwa watapata suluhu kwa utata unaozingira kuajiriwa kwa Naibu wa Chifu wa eneo hilo.
Kwa sasa Naibu Chife wa eneo hilo la Gesure anasemekana kuajiriwa kwa njia isio ya haki ila kufuata ukoo wa nyumba fulani.
Akizungumza afisini mwake siku ya Jumatano, Kamishna Mwangi alisema atazuru eneo hilo hivi karibuni kutatua suluhisho kwa malalamishi ya wakaazi hao.
Hii ni baada ya wakaazi wa eneo hilo la Gesure wakiongozwa na kiongozi wao David Ogega kuandamana hadi ofisini mwake hapo jana Jumatano wakilalamikia kuajiriwa kwa Naibu Chifu huyo wakidai kuwa zoezi hilo ni la ufisadi.
“Mwenye alichaguliwa anatoka Ukoo moja na Chifu wa eneo hili pamoja na Mwakilishi wa Wadi ya eneo hili. Wote ni wa Ukoo moja kwani ukoo zingine hazina watu wakufuzu?,” alisema Ogega kiongonzi wa walioandamana.
“Tulikuja kwa kamishena wetu akuje mpaka kule Sameta atatue shida hii maana tunaumia sana ni usaidizi tulikuja kutafuta maana hatuwezi vumilia kuongozwa na Ukoo moja kwani watu wengine hawakusoma?,” aliuliza Ogega.
Wakaazi hao walisema kuwa wameiweka rasmi kwa Kamishena Mwangi kuwa hawajafurahishwa na zoezi hilo. Kilio chao sasa kitashughulikiwa kwani Kamishna huyo atazuru sehemu hizo ili kusuluhisha utata huo.