Kamishna wa kaunti ya Kisumu Erastus Ekidor amehakikisha kuwa usalama wa kutosha utahimarishwa hapo kesho, wakati mwili wa mwanae alieyekuw wazir mkuu Raial Odinga Fidel utakapowasili jijini Kisumu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ekidor amesema maafisa wa usalama watashika doria katika kila pembe, ili kuona kuwa hali ya usalama inadumishwa kwenye hafla hiyo, pindi mwili utakapowasili katika uwanja wa ndenge wa kimataifa wa Kisumu na kupelekwa katika uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta jijini Kisumu kwa wananchi kuutazama kisha kusafirishwa Bondo katika kaunti ya Siaya.

Ekidor amewataka wakaazi wa Kisumu wawe na nidhamu wakati watapewa fursa ya kuutazama mwili wa mwenda zake Odinga.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani Kisumu Moses Ole Tutui amesema tayari mipango ya usalama wa hapo kesho imekamilika, na kuwataka wakaazi wa Kisumu wawe na nidhamu wakati mwili wa Fidel utakapowasili.

Fidel alipatikana amefariki nyumbani mwake Karen siku ya Jumapili iliyopita, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha kifo chake.