Kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini, kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amejitokeza kuwarahi wakazi wa kaunti hiyo kutahadhari. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mahojiano ya kipekee siku ya Jumatano, Onunga alisema kuwa yafaa wakazi wanaoishi katika maeneo ya nyanda za chini watahadhari. 

"Mvua nyingi inaendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini, na ni himizo langu kwa wakazi wanaoishi kwenye maeneo ya nyanda za chini hasa Esise na Nyansiongo kutahadhari kwa kuhamia nyanda za juu," alisema Onunga. 

Onunga aidha aliwahimiza wakazi wa kaunti ndogo ya Borabu kushirikiana na maafisa wa polisi ili kusaidia kuthibiti visa vya wizi wa mifugo. 

"Kwa muda sasa kumekuwa kukiripotiwa visa vya wizi wa mifugo mpakani Borabu, na kwa kweli maafisa wa polisi hawawezi kuthibiti hali hiyo bila ya ushirikiano wa wananchi," aliongezea Onunga.