Kwa mara nyingine tena kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amejitokeza kuwaonya vikali madereva dhidi ya kutozingatia sheria za barabarani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu mapema Jumanne, Onunga alisema kuwa ajali nyingi hutokea kutokana na kutozingatiwa kwa sheria za barabarani na baadhi ya madereva. 

"Ajali nyingi hutokea kwa sababu ya kuwepo madereva wasiozingatia sheria za barabarani, na sharti shera zichukuliwe dhidi ya wale watakaopatikana wakiuka sheria za trafiki," alisema Onunga. 

Onunga aidha aliwataka wamiliki wa magari kuhakikisha kuwa magari ya usafiri yanayohudumu barabarani ni magari yanayostahili. 

"Kwa kweli ili tuweze kukabili visa vya ajali kwenye barabara sharti wamiliki wa magari ya usafiri wahakikishe kuwa magari yanayohudumu barabarani yako kwenye hali nzuri." aliongezea Onunga.