Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amejitokeza kuwahimiza madereva kuwa waangalifu kwenye msimu huu likizo za pasaka. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mahojiano ya kipekee mapema Ijumaa, kamishna Onunga alisema kuwa sharti madereva wawe waangalifu barabarani ili kulinda maisha ya wasafiri.

"Tumeanza sherehe za msimu wa pasaka na ni ombi langu kwa madereva kuwa waangalifu zaidi barabarani kwa kuzingatia sheria na masharti ya idara ya trafiki ili kulinda maisha," alisema Onunga. 

Onunga aidha aliwaonya vikali watu walio na nia ya uhalifu akihoji kuwa maafisa wa polisi watakuwa macho kuhakikisha kuwa wakazi wa kaunti ya Nyamira wanasherehekea pasaka bila matatizo yeyote. 

"Jukumu la maafisa wa polisi ni kulinda usalama miongoni mwa wananchi, basi na yeyote aliye ba nia ya kujihuzisha na visa vya uhalifu kwenye msimu huu wa pasaka wacha ajue kwamba tutakabiliana naye kwa maana maafisa wa polisi watakuwa macho kuhakikisha kila mtu anasherehekea pasaka bila matatizo," aliongezea Onunga.