Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Bwana Thomas Letangule ameusuta muungano wa Cord kwa kutaka majadiliano yaanzishwe kuhusu tume hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea wakati alipokuwa akihojiwa na Aljazeera siku ya Jumatano, Bwana Letangule alisema kuwa mrengo wa upinzani hauna haja na marekebisho ya tume hiyo.

Alidai kuwa lengo lao kuu ni kushindania mamlaka.

Aidha, kamishna huyo aliwakosoa viongozi wa Cord kwa kufanya sherehe sambamba za siku ya Madaraka katika bustani ya Uhuru, jijini Nairobi.

"Kile kinachoshuhudiwa Kenya kwa sasa ni ushindani wa nguvu za kisiasa na mamlaka. Kuna madhumuni makuu sana katika haya mnayoyashuhudia hasa kisiasa,” alisema Letangule.

Aliongeza, "Cord wako kwa hali ya taharuki na mshtuko tunapoelekea uchaguzi mkuu. Hiyo ndio maana unaona shutuma za kila aina zikirushwa kila mahali hasaa dhidi ya Tume ya IEBC,” alisema kamishna huyo.