Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amejitokeza kuwaonya vikali wazazi dhidi ya mazoea ya kuwaficha watoto walio na ulemavu manyumbani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu mapema Jumanne, Onunga alisema kuwa yeyote atakayepatikana akiwafungia watoto walio na ulemavu manyumbani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wazazi wanaowafungia watoto walemavu nyumbani bila kuwaruhusu kutangamana na wenzao," alionya Onunga. 

Afisa huyo pia aliwaonya vikali wanaoendeleza ugemaji wa pombe haramu huku akiwataka machifu kuangamiza ugemaji wa pombe hiyo. 

"Serikali ingali inazidisha vita dhidi ya ugemaji wa pombe haramu, na ni wajibu wa machifu na manaibu wao kuhakikisha kuwa ugemaji na unywaji wa pombe haramu unaangamizwa," aliongezea Onunga.