Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Maalim Mohamed amepewa uhamisho wa ghafla hadi Kaunti ya Kisumu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Kamishna wa Kaunti ya Muranga Evans Achoki.

Akithibitisha uhamisho huo, Maalim alisema amefanya jukumu lake kama kiongozi kwa mujibu wa katiba katika kipindi cha miezi miwili aliyohudumu Mombasa.

Aidha, aliongeza kuwa hakuna atakayetambua juhudi zake isipokuwa wakaazi wa Mombasa, ambao ndio walishuhudia utendakazi wake.

Maalim alikuwa ameapa kuyaangamiza makundi haramu eneo nzima la Mombasa.

Kwa ushirikiano na idara ya usalama, alifanikiwa kuwaua wahalifu 10 katika kipindi cha miezi miwili.

Kaunti ya Mombasa inatambulika kwa makundi ya uhalifu kama vile Wakali Wao, wakali Kwanza, Born to kill na Kapenguria six.