Kamishna wa kaunti ya Nakuru Joshua Nkanatha ametoa wito kwa maafisaa wa polisi kufanya misako na uchunguzi ili kuwakamata watu ambao wanaendeleza biashara haramu ya kuuza mafuta ya petroli na diseli.
Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumamosi, Nkanatha alisema amepokea ripoti kutoka kwa umma kwamba kuna watu ambao hufyonza mafuta kutoka kwenya malori yanayosafirisha petroli kupitia barabara kuu za eneo hilo.
Nkanatha amesema kuwa kundi hilo la watu linazidi kuyahatarisha maisha ya wakaazi kwani mafuta hayo hufichwa kwenye makazi.
Aidha amewatahadharisha pia madereva wa malori hayo ambao wanashirikiana na wanunuzi hao, kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mtu mmoja alifariki mnamo Disemba 5, 2015, wakati wa ambapo lori moja liliteketea na kudai mkasa huo ulitokana na ufyoonzaji wa mafuta.