Imebainika kwamba maambukizi ya funza hapa pwani yamepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na kitengo cha afya ya umma kaunti ya Kilifi, kaunti za pwani zilizokuwa zinakumbwa na wadudu hawa zimepewa dawa ya kutibu wadudu hao huku wakaazi wakihamasishwa kila uchao kuhusiana na umuhimu wa usafi.

Afisa mkuu wa kitengo hicho Dkt John Karanja alisema idadi ya wanaoathirika na wadudu hao imeonekana kupungua kwa kiasi kikubwa huku akisema funza wamekuwa wakiwavamia wazee hata watoto wachanga na kuwaacha na mashimo kwenye vidole vyao huku wengine wakishindwa hata kutembea kutokana na vidondo ambavyo imma hutoa majimaji yaliyouchungu.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuwatibu funza wakaazi wa kijiji cha Mijikenda huko Malindi, Dkt Karanja ameyataja maeneo ya Kwa Chocha, Kijiwetanga, Kwa Upanga miongoni mwa maeneo mengine ambayo yameathirika zaidi na funza, na kuongeza kwamba maambukizi ya funza huzidi wakati wa kiangazi.

Waathiriwa wa funza hata hivyo wametahadharishwa dhidi ya kutumia mbinu za zamani kutibu funza ikiwemo utumiaji wa vijiti, akisema njia hizo zimesababisha kuenea kwa wadudu hao.

Hata hivyo ameziomba kaunti za pwani kushirikiana na kuendelea kutoa huduma za matiba kwa wakazi wanaokabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame akisema kuwa wadudu hao hupenda kuvamia msimu huu.