Kanisa katoliki hapa nchini linaunga mkono mabadiliko ya mtaala wa 8,4,4.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kupitia kwa mwenyekiti wa tume inayoshughulikia maswala ya elimu na elimu ya kidini katika baraza la maaskofu wa kanisa katoliki hapa nchini KCCB, askofu Maurice Muhatia Makumba, kanisa katoliki linasema zoezi hilo linaloendelea kwa sasa ni muhimu katika jamii na hata taifa zima kwa ujumla na kizazi cha siku zijazo.

Hata hivyo ametoa wito kwa umma kufuatilia mchakato huo wote kwa makini na hata mfumo wa elimu unavyoendeshwa na maswala ya mitihani.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na waalimu wakuu wa shule zilizo chini ya uongozi na udhamini wa jimbo katoliki la Nakuru katika eneo La St Marys Pastoral Centre Mjini Nakuru wiki iliyopita.

‘Ingawa zoezi hilo ni muhimu kwenye na katika Jamii, ni muhimu pia kwetu kuangazia jinsi ya sekta ya elimu hapa nchini inayoendelezwa," alisema askofu Muhatia.

Kwa upande wake, msaidizi wa askofu katika jimbo katoliki la Nakuru vicar general padri Lawrence Mbogo ambaye pia alihudhuria mkutano huo alifafanua zaidi kuhusiana na umuhimu wa zoezi hilo la kubadili mtaala akisema linalenga kuhakikisha ukuzaji ulio kamili kwa mwanafunzi. 

Licha ya hayo, amesisitiza kwamba ni muhimu kuzingatia kuhusiana na maswala yatakayoongozwa kwenye mtaala huo na yale yatakayotolewa ili kuhakikisha kuwa mwanafunzi anapata ukuzaji huo.

Mfumo wa 8,4,4 unanuiwa kubadilishwa na hadi ule wa 2,6, 6,3 ambao wanafunzi watasoma miaka 2 kwenye shule ya chekechea,miaka 6 katika shule ya msingi,miaka 6 kwenye shule ya upili na miaka mitatu katika chuo kikuu.

Vilevile mfumo huo, ulioanzishwa mwaka 1985 unalenga kutupilia mbali mitihani ya kitaifa na kuwapa wanafunzi nafasi ya kusomea kazi zenye mvuto mkubwa kwao wakiwa bado katika shule ya upili.