Naibu Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo kuu la Mombasa Padri Wilbard Lagho amewaomba viongozi wa kisiasa katika eneo la Pwani na Kenya kwa jumla kusitisha siasa za chuki na malumbano kuzuia ghasia.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungmza mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Padri Lagho amesema kuwa kila Mkenya ana haki kikatiba kujitosa katika ulingo wa kisiasa lakini swala muhimu la kuzingatia ni uiano na uutangamano wa jamii badala ya kuchangia siasa za chuki.

Amewataka viongozi wa kisiasa, wakaazi na jamii kwa jumla kuhakikisha kuwa wanajitenga na siasa za chuki na uchochezi ambazo huenda zikawagawanya Wakenya katika misingi siofaa nchini huku akisisitiza kudumishwa kwa amani na utangamano wa jamii.

“Tunawaomba viongozi wa kisiasa, wakaazi na jamii kwa jumla kuhakikisha kuwa wanajitenga na siasa za chuki, malumbano na ukabila hata kidini na badala yake wawe viongozi wa kupenda kueneza amani mashinani ili Wakenya waishi bila mafarakano,” alisema Padri Lagho.

Mapendekezo ya kiongozi huyo wa kidini yamejiri huku Wakenya wakijiandaa katika uchaguzi mkuu ujao, swala kuu ikiwa kudumisha amani na utangamano wa jamii nchini.