Askofu Maurice Muhatia Makumba wa kanisa katoliki dayosisi ya Nakuru ametoa with Kwa wakristo na Manisa Kwa jumla kukumbatia miradi ya maendeleo kwani itakuwa ya manufaa hata kwa kizazi kijacho.
Alisema hayo Jumamosi wakati wa hafla ya mchango wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa jengo la vyumba vya malazi.
Mradi huo upo chini ya muungano wa wanawake wakatoliki CWA, na Askofu Muhatia aliwataka wakristo kufahamu kwamba mradi huo ungewasaidia si wao tu pekee bali pia kizazi kijacho.
"Tumekusanyika hapa kuchanga fedha za mradi huu wa akina mama, lakini ni lazima tujue ni mradi utakaofaidi hata kizazi kijacho wakati sisi tumezeeka," alisema Askofu Muhatia.
Wakati huo huo, alisisitiza umuhimu wa familia katika misingi ya kanisa, huku akiwataka akina mama kusimama imara na familia zao.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba mradi huo wa ujenzi utafanyika mkabala na kituo cha St Mary's Pastoral Centre Nakuru.
Picha: Askofu Maurice Muhatia Makumba wa kanisa katoliki dayosisi ya Nakuru. Amewataka wakristo kukumbatia miradi ya maendeleo kanisani.PMambili/Hivisasa.com