Kinara wa Chama cha Narc Kenya amewataka wanawake katika eneo la Pwani kutokubali kununuliwa na wanasiasa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika kongamano la kuwahamasisha wanawake kuhusu uongozi lililoandaliwa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar katika kituo cha Renaissance jijini Mombasa, Martha Karua aliwataka wanawake kutokubali kupewa pesa ili kupigia kiongozi yeyote kura.

“Msikubali kushawishiwa kwa pesa ili kupigia kiongozi kura. Chagueni viongozi kwa vitendo na maendeleo waliyoleta wala sio kwasababu ya pesa,” alisema Karua.

Karua alisema sharti wanawake wawe na mipango na maono ya jamii na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi sawa na wanaume.

Aidha, amewataka wanawake kuwa macho na siasa za nipe nikupe ambazo zimekita mizizi nchini.