Wakaazi wa kaunti ya Nakuru wametakiwa kulikumbuka taifa katika maombi ili kumaliza migogoro.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumapili katika kanisa la PCEA kasisi Arthur Ndegwa alisema baadhi ya changamoto za taifa zinaweza kutatuliwa iwapo wakenya watajikita katika maombi.

"Hizi shida tunaskia kila mara zitaisha tu iwapo tutaomba zaidi" kasisi Ndegwa alisema.

Wakati huo huo, amewapa changamoto wakristo kutojihusisha na ufisadi bali wawe kielelezo chema katika jamii. 

"Ufisadi upo lakini wakristo tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa hatujihusishi na swala hili," Ndegwa alisema.

Naye kasisi George Wamani wa dhehebu hilo la PCEA alitoa wito kwa viongozi wa kidini kuzidi kupeana mwelekeo kwa serikali.

"Viongozi wa kidini tuna wajibu mkubwa wa kupeana mwelekeo kwa serikali" alisema Wamani.