Vijana katika eneo bunge la Kabete wametahadharishwa dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa wakati huu wa kampeni kumchabua mbunge wa eneo hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea katika ibaada maalum ya vijana katika kanisa la Glory to Jesus Tabernacle mtaa wa Gikuni, mhubiri Francis Mukabana alisema kuwa vijana hapo awali wametumiwa kutekeleza maovu wakati wa kampeni jambo ambalo ni hatia.

“Nawahisi vijana muwe wenye hekima na wenye kutilia maanani yale tunayowaonya. Siasa si mbaya lakini mnapo anza kutumiwa kuwadangaya watu, kuwapiga ama kukejeli wagombeaji wengine kimatusi si vyema machoni pa Mwenyezi Mungu,” alieleza Mukabana.

Aliendelea kwa kusema kwamba vijana wananaswa haraka na wanasiasa kwa kuwa wengi hawana mapato na kwa sababu hii wanamalizia kutumiwa vibaya.

“Vijana mnafaa kujihusisha na shughuli halali na inayomtukuza Mungu kutafuta mapato na hata hivyo mwaweza ungana katika vikundi na kufanya michango ambayo mnaweza tumia kufanya biashara,” alisema.

Alifafanua kwamba wengi wa vijana hapo awali wametumika kuleta fujo katika mikutano ya washindani wa wanaowatekelezea kazi, udanganyifu wa taarifa kuhusu wagombeaji wengine, na hata kutumika kuwahonga wapiga kura.

Kiongozi wa vijana katika kanisa hilo bwana Fredrick Uhuru alisema kuwa neno hilo lilikuwa la manufaa kwao hususan kwa wale ambao walifikiri kuwa uovu wa kisiasa hauna dhambi.

“Mungu ndiye muumba wa mbingu na ardhi na ni dhambi kupuuza neno la Mungu ili kuweza kumfurahisha binadamu,” alieleza kiongozi wa vijana.