Mwakilishi wa wadi ya Mjambere Fahad Kassim. [Photto/standardmedia.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa wadi ya Mjambere Fahad Kassim amesema kuwa kulikuwa na jaribio la kuuawa kwake baada yake kuulizia pesa za maendeleo za wadi.

Fahad Kassim alisema pia hatua hiyo ilitokana na hatua yake kuulizia ni kwa nini wakilishi wadi hawajapewa mikopo ya kununua magari.

Mwaka wa 2014 mwezi machi rais Uhuru Kenyatta alipendekeza  kuwa wakilishi wadi wapewe mikopo ya kununua magari kama wanavyopewa Wabunge na Maseneta akihoji kuwa wakilishi wadi ni viongozi waliochaguliwa na wakenya. 

Kassim alisema kuwa tarehe 25 mwezi uliopita alifuatwa na magari matatu jambo ambalo alisema kuwa si la kawaida. 

"Tukio hilo lilifanyika karibu na eneo la Nyali ambapo abiria way ale magari walikuwa na nia ya kunidhuru, “Alisema Kassim.

Kassim ambaye ana leseni ya kumiliki bunduki alisema kuwa hakufanya chochote kwa sababu hakujuwa iwapo polisi walikuwa ndani mwa yale magari au la.

Kulingana na Kassim, wakilishi wadi wa Mombasa walikuwa wametishia kulemaza shughuli za bunge la kaunti ya Mombasa iwapo malalamishi yao hayangesikizwa.

Kassim aliongeza kuwa ni kaunti ya Mombasa pekee ambayo haijapata fedha za maendeleo za wadi.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published.* https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF