Jimbo la Nakuru limepanga kuwaajiri wanfanyakazi wa afya ili kukidhi upungufu wao kaitka hospitali.
Akiongea siku ya Ijumaa akiwa Gilgil kwenye hafla ya Gavana Mtaani, gavana Kinuthia Mbugua alisema kwamba walikua wametangaza nafasi za kazi pamoja na zile za madaktari.
"Suala la upungufu wa wafanyakazi ni changamoto kwa jimbo hili na pale tutakapoajiri watu, tatizo hili halitakua tena."
Mbugua alisema hospitali zimeongezwa na hivyo wafanyakazi wanahitajika kwa uwingi.
“Tunafahamu kwamba tunahitaji kuongeza madakatri na wafanyakazi wengine katika hospitali hizi mpya na kwa hivyo, mradi huu wa kuajiri watu utakua wa haki," aliongezea Mbugua.