Gavana Granton Samboja (kulia) akiwa na afisa mkuu wa kampuni ya Equatorial Nuts Company Joseph Muzuzi (katikati) katika afisi ya gavana huko Wundanyi. [Picha/Eddie Nyange]

Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta imetangaza kukifufua tena kiwanda cha macadamia cha Horticultural Production Centre (HTS), kilichoko Wundanyi ili kuinua kilimo.Akidhibirisha haya baada ya kikao na maafisa kutoka kiwanda cha Equatorial Nuts Company kutoka Kaunti ya Murang'a, Gavana Granton Samboja ameitaja hatua hiyo kama njia moja wapo ya kubuni nafasi za ajira kwa wakaazi wa kaunti hii hasa vijana ambao wengi wao hurandaranda mitaani kwa kukosa ajira.Samboja alisema kiwanda hicho pia kitaboresha uchumi wa kaunti hiyo na kupigana na swala la mawakala ambao kwa muda mrefu wamekua wakiwalaghai wakulima."Furaha yetu kuu kama wawakilishi wa wananchi hawa ni pale tutakapoona wakifanikiwa hasa kutokana na kilimo hiki kwa kuwa watu wengine pia watavutiwa na pia wajiunge na kilimo," alisema Samboja.Mwenyekiti wa kamati ya ukulima na ufugaji katika bunge la Kaunti ya Taita Taveta Juma Mwamba amepongeza hatua hiyo na kuongeza kuwa itasaidia wakulima kukwepa kuvuna mazao kabla hayajakuwa tayari."Wakulima wetu sasa watapewa mafunzo ya kuboresha kilimo chao na kuepuka kuvuna mazao ambayo hayajakomaa na mwishowe kukosa soko," alisema Mwamba, ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Wusi/Kishamba.Afisa mkuu wa kampuni ya Equatorial Nuts Company Joseph Muzuzi alisema kuwa wataweka mikakati ya kuwalipa wakulima kupitia kwa vyama vya ushirika ili kuwaepusha na walaghai."Tunajadiliana kuhusu mbinu mwafaka ambazo wakulima watatumia ili kupata mazao ya kutosha, na jinsi ya kuwalipa pesa wanapouza mazao yao ili kuepuka malalamishi," alisema Muzuzi.Zaidi ya miche 5,000 imetolewa na kampuni hiyo na inatarajiwa kupandwa katika kituo cha kilimo cha ATC – Ngerenyi, kabla ya kusambazwa kwa wadi nne zilizotengewa mradi huo.Wadi hizo ni Wusi/Kishamba, Werugha, Wumingu/Kishushe na Mwanda/Mghange.