Serikali ya kaunti ya Nyamira imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wagonjwa wa kifua kikuu wamepata huduma bora ya matibabu ili kuzuia vifo kupitia ugonjwa huo.
Haya yanajiri baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa ugonjwa huo wa kifua kikuu ni ugonjwa namba nne kwa mauaji katika taifa la Kenya.
Kulingana na waziri wa afya katika kaunti ya Nyamira Gladys Momanyi, aliyezungumza mjini Nyamira, serikali ya Nyamira itahakikisha wagonjwa wa aina hiyo watapata huduma bora katika hospitali za kaunti hiyo ili kuzuia maafa mengi.
“Ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa ambao umetambulika kuwa namba nne katika mauaji, na serikali ya Nyamira imeweka mikakati ya kutoa huduma bora za ugonjwa huo katika hospitali za Nyamira,” alisema Momanyi.
Kwa upande wa daktari mkuu katika kaunti hiyo Jack Magara aliomba wakazi kufika katika hospitali mapema ili kutipiwa kabla ya uongwa huo kuenea mwilini zaidi
“Heri mgonjwa kupata tiba mapema kuliko kusubiri ugonjwa huo kuenea zaidi mwilini. Naomba wakazi wakiona dalili za ugonjwa huo kufika hospitali ili kupata tiba,” alisema Dkt Magara.