Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa inanuia kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya udaktari katika vyuo vya kadri.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mradi huo ambao utagharimu shilingi milioni 25 katika kipindi cha miaka mitano unatarajiwa kufaidi zaidi ya wanafunzi 35 wasiojiweza kifedha.

Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya Afya Mohammed Abdi, mradi huo utafanikishwa kwa ushrikiano na shirika lisilo la serikali la USAID.

Aidha, alisema watakaofaidika na mikopo hiyo watatakiwa kuilipa baada ya kuhitimu masomo yao.

"Ni mkopo utakaozunguka baina ya wanafunzi. Mwanafunzi atakapohitimu atalazimika kulipa ili wengine waje kufaidika pia," alisema Bi Carole Karutu, afisa wa mradi huo.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya serikali ya kaunti kutoa ufadhili wa asilimia 70 wa kielimu kwa vijana katika maeneo tafouti.

Mpango huo utajumuisha taaluma ya teknolojia ya mawasiliano, utengezaji wa filamu, lugha ya ishara, miongoni mwa zingine.