Waziri wa kilimo kaunti ya kisii, Vincent Sagwe, amesema serikali ya  kaunti hiyo imeweka mikakati kabambe ya kufungua kiwanda kipya cha maziwa mjini Kisii. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza hii leo katika ukumbi wa kitamaduni  [Kisii cultural hall] Sagwe alisema kuwa serikali ya Kisii imejiandaa kujenga kiwanda cha maziwa.

”Tutajenga kiwanda cha maziwa hivi karibuni ,na ninawaomba wakulima wote hasa wale wa kufuga ng’ombe wa maziwa tukimaliza ujenzi wa kiwanda hicho watuletee maziwa yao na tutawalipa vizuri,” akasema Sagwe

 Aidha, waziri huyo alisema kiwanda cha parachichi kilichojengwa katika kaunti hiyo, kitapanuliwa.

Sagwe alisema kuwa serikali hiyo imetenga pesa za kuendeleza miradi ambayo itasaidia wakulima wa eneo hilo.

Waziri huyo alihoji kuwa kiwanda cha parachichi kilichoanzishwa katika kaunti hiyo kimeanza kutengeneza mafuta ya kujipaka. 

"Pesa ambazo tunapata kutoka kwa mradi huo zinasaidia kuendeleza maendeleo," alihoji Sagwe.

Kaunti ya Kisii iliongoza kwa sekta ya kilimo katika utafiti uliofanywa na kampuni ya  infor track.