Hospitali ya Kisii kwa ushirikiano na madkatari wa hospitali ya chuo cha Aga khan, kutoka Nairobi, wameanza kupima wakazi wa kaunti ya Kisii ugonjwa wa saratani ya matiti bila malipo.

Share news tips with us here at Hivisasa

 Akiongea hii leo (Jumatatu) katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kisii Daktari mkuu ambaye anasimamia shughuli hiyo Raymond Oigara alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia watakaopatikana wameadhiriwa na ugonjwa huo kwani watatibiwa bila malipo.

“Ugonjwa wa saratani umewaua watu wengi sana nchini; kwa sasa umeorodheshwa kama moja ya ugonjwa unaoua watu wengi nchini,” akasema Oigara.

 “Zoezi la leo ni njia moja ya kupima na kuwafunza wamama jinsi watakapojipima wao wenyewe hata wakati wako nyumbani mwao,” aliongezea Oigara.

Wanawake wengi waliojitokeza katika shughuli hiyo ikilinganishwa na wanaume. 

 Darktari Shahin Sayed Mohamed kutoka Aga khan amesema waliojitokeza ni watu 300  huku wanaume wakiwa watatu.

Mohamed aliwaomba wanaume kujitokeza ili kupimwa ili kujua hali yao kwani hata wao huadhiriwa na ugonjwa wa saratani ya matiti.

“Mara mingi ugonjwa huu wa saratani huwapata wa mama lakini wanaume pia huadhiriwa nao,” asema Mohammed.

Mohammed aliongeza kuwa wakati huu namba ya wale wameathiliwa iko chini ikilinganisha na wakati huo mwingine walipoliendeleza shughuli hiyo.