Serikali ya kaunti ya Lamu imethibitisha kupokea kwa vifaa vya matibabu vya gharama ya shilingi milioni 37 kutoka kwa wafadhili wa hazina ya umoja wa mataifa.
Akizungumza na wanahabari kwa njia ya simu siku ya Jumatano, Mkurugenzi wa mawasiliano katika kaunti ya Lamu, Linda Mboya amesema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na vile vya kuwasaidia akina mama kujifunguwa wakati wa ujauzito.
Linda amesema kuwa vifaa hivyo tayari vimesambazwa katika hospitali tatu katika kaunti hiyo ikiwemo hospitali ya Faza, Mpeketoni na Kipfahad ili kuhakikisha kuwa wakaazi wa kaunti ya Lamu wanapata matibabu bora.
"Tumepokea ufadhili huo na tayari tumezambaza baadhi ya vifaa hivyo kwa hospitali tatu zile ambazo tunajua wakaazi wa Lamu wanapitia changamoto ili kuzuia kushughudiwa kwa maafa kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu licha kama kaunti tuko na mikakati ya kuimarisha zaidi sekta ya afya katika kaunti yetu," alisema Linda.
Hata hivyo amewahimiza wakaazi hasa akina mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanavitembea vituo vya afya kupata usaidizi zaidi wakati wa kujiufungua ili kuwalinda watoto wao dhidi ya kupata maradhi ya kiafya.