Kaunti ya Machakos imeorodheshwa kuwa bora katika utendakazi ikilinganishwa na Kaunti zingine hususan katika maswala ya ugatuzi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya Infotrak Harris kati ya mwezi Disemba mwaka uliopita na Februari mwaka huu.

Kwenye utafiti huo asilimia zaidi ya 61 ya watu 28,000 waliohojiwa walielezea kuridhishwa na huduma za Afya, Elimu, Kilimo, uboreshaji wa mazingira pamoja na kuimarishwa kwa miundo msingi.

Kaunti ya Bungoma ilinyakua nafasi ya pili kwenye utafiti huo ikifuatwa kwa karibu na Kaunti ya Vihiga.

Kaunti zingine zilizo oredheshwa kwa utendakazi bora ni Bomet, Kwale, Elgeyo Marakwet, Taita-Taveta, Kisii, Pokot Magharibi, Kakamega, Kericho, Murang’a, Nandi, Uasin Gishu na Mombasa.

Aidha Kaunti zote zilizoko eneo la Nyanza hazikuorodheshwa isipokua Kisii miongoni mwa Kaunti 15 zinazotekeleza kiukamilifu swala la ugatuzi na kutoa huduma za kuridhisha wenyeji.

Hili linaacha maswali mengi kuwa ni vipi Kaunti hiyo hufanikisha haya yote ikizingatiwa kwamba Kaunti ya Machakos sio miongoni mwa Kaunti ambazo hupokea mgao mkubwa wa fedha.

Hivi maajuzi, tume ya kupambana na ufisadi iliwataja Magavana kadhaa kwa tuhuma za ufisadi. Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua alikuwa miongoni mwao. Licha ya hiyo Gavana huyo ndio kiini cha haya mafanikio yote ya Kaunti ya Machakos.