Wakazi katika shamba la Waitiki eneo la Likono wamepata afueni kubwa baada ya bunge la serikali ya kaunti ya Mombasa kupitisha mswada wa kuwalipia ada za kumiliki shamba hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Siku ya Alhamisi, wawakilishi wa bunge la Mombasa walipitisha hoja ya kusimamia ulipaji kwa shamba hilo kwa miaka 23 pasi mwanchi wa eneo hilo kutoa hata ndururru kama walivyotakiwa na serikali kuu.

Hoja hiyo iliwasilishwa bungeni na mwenyekiti wa kamati ya fedha Mohamed Hatimy, ambapo alisema serikali ya Kaunti ya Mombasa italipa ada hizo kwa muda wa miaka 23 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.25.

Mswada huo sasa utafikishwa kwa gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho kama inavyoelekeza sheria.