Serikali ya kaunti ya Mombasa imeshikilia kuwa itashirikiana kwa karibu mno na Halmashauri ya ukadiriaji ubora wa bidhaa nchini KEBS kuhakisha kuwa kampuni zote zinazotengeza maji ya chupa katika kaunti ya Mombasa zinachuguzwa iwapo zinafikia viwango vya biashara hiyo.
Waziri wa Afya kaunti ya Mombasa Mohamed Ibrahim Abdi amesema kuwa baadhi ya kampuni katika kaunti hiyo zinauza maji ya chupa yasifikia viwango hitajika vya kiafya na huenda ikachagia madhara ya kiafya ikiwemo kuongezeka kwa ugonjwa wa Homanyongo katika kaunti hiyo.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Abdi amesema kuwa uchunguzi wa kampuni hizo uendelea na iwapo kampuni nyingi itapatika basi zitafungwa ili kuzuia kuchipuka kwa magonjwa mbalimbali ya kiafya huku akiwataka wakaazi kuwa waangalifu dhidi ya kutumia maji kiholela.
"Tunashirikiana na KEBS kuhakikisha kuwa kampuni zinazotengeza maji ya chupa Mombasa bila idhini tunazichukulia za kisheria ili kuzuia kuenea kwa maradhi ya kiafya kwa wakaazi wa Mombasa," alisema Abdi.
Kampuni zilizofungwa ni pamoja na ile ya Bamba iliyoko eneo la Nyali, Zeit eneo la Kisauni, Zahra Cool eneo la Ganjoni, Sundus eneo la Majengo na Active eneo la Bombululo zote zikiwa katika kaunti ya Mombasa.