Wafanyibiashara katika Soko la Kongowea, Marikiti na Mwembe Tayari mjini Mombasa wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa chini ya uongozi wa Gavana wa kaunti hiyo Ali Hassan Joho kukarabati masoko makuu Mombasa ili kuimarisha shughuli za kibiashara.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongozwa na Katibu wa Chama cha Wafanyibiashara wa Soko la Kongowea Peter Nyaga, wafanyibiashara hao wamesema kuwa serikali ya kaunti hiyo inafaa kutenga kiasi cha fedha katika bajeti mwaka wa 2016/2017 zitakazotumika katika kukarabati masoko makuu ili kuekeza zaidi.

Nyaga amesema kwamba kutokana na mazingira duni ya masoko hayo pamoja na kuwepo na mirundiko ya taka karibu na masoko hayo kumechangia kuwepo na biashara duni hali ambayo inachangia kudorora kwa uchumi wa nchini.

“Tunamuomba gavana Joho na serikali yake kuhakikisha kuwa masoko ya Mombasa yanafanyiwa ukarabati hususan Soko la Kongowea, Marikiti na Mwembe tayari angalau kusaidia kuboresha shughuli za kibiashara kwani masoko haya ncdio yanayotegemewa na wakaazi wote wa afrika masharaki,” alisema Nyaga siku ya Jumapili katika mkutano wa wafanyibiashara mjini Mombasa.

Wafanyibiashara hao washinikiza viongozi wa kaunti ya Mombasa hadi mazingira ya masoko hayo kuboreshwa mjini humo.